SUALA LA AIRTEL MIKONONI MWA RAIS,WAZIRI WA AFYA NA SHERIA NAO WATEKELEZA MAAGIZO YA RAIS
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Isdor Mpango leo amewasilisha
taarifa ya kamati aliyoiunda kuchunguza umiliki wa kampuni ya simu Airtel kwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli aliyeagiza
kufanyika kwa uchunguzi huo Desemba 20 mwaka jana.
Dkt.Philipo Mpango |
Kufuatia ukiukwaji huo Dkt.Mpango amesema Serikali
inayomiliki asilimia 40 ya hisa za kampuni ya Airtel imeamua kufanya mazungumzo
na kampuni ya Airtel inayomiliki asilimia 60 ya hisa ili nchi iweze kupata haki
yake.
Dkt.Ummy Mwalimu |
Miongoni mwa maagizo hayo ni kupunguza baadhi ya idara na
madaktari katika hospitali ya Taifa Muhimbili na kuhamishia Mloganzila na
hospitali za mikoa,kuhamishwa kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (TAMISEMI) kwenda Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee
na Watoto.
Mhe.Ummy Mwalimu amewasilisha taarifa hiyo akiwa ameongozana
na viongozi wakuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,Taasisi ya Mifupa
(MOI),Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKHI),Chuo Kikuu cha Tiba na
Sayansi Shirikishi (MUHAS).
Katika hatua nyingine,Waziri wa Katiba na Sheria Prof.
Palamagamba Kabudi amekamilisha kanuni za sheria ya madini namba 7 ya mwaka
2017 na kuwasilisha vitabu vya kanuni hizo kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John
Kijazi.
Prof.Palamagamba Kabudi |
Kwa upande wao Naibu Mawaziri wa Madini wamewataka Watanzania
na wadau wote wa sekta ya madini kushirikiana na Serikali kutekeleza sheria
hiyo na wamempongeza Mhe.Rais Magufuli kwa kutoa msukumo wa kukamilishwa kwa
kanuni hizo.
Habari zaidi ni
P5TANZANIA LIMITED
Comments