MTOTO MCHANGA WILAYANI MPANDA MKOANI KATAVI AOKOTWA NA WATOTO AKIWA AMETELEKEZWA NA MAMA YAKE

Na.Issack Gerald
Mtoto mchanga anayekadiriwa kuwa na umri kati ya mwezi mmoja mpaka mitatu Wilayani Mpanda Mkoani Katavi ameokotwa akiwa ametelekezwa na mama yake mzazi ambaye hata hivyo hajatambulika.
Kuokotwa kwa mtoto huyo wa jinsi ya kike kumethibitishwa na Afisa ustawi wa jamii Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Bi.Redigunga Mayorwa ambaye amesema mtoto huyo ameokotwa na watoto waliokuwa wakicheza katika mtaa wa Airtel kata ya uwanja wa Ndege.
Bi.Mayorwa amesema watoto waliomuokota akiwa amefunikwa majani ambapo walimpeleka kwa wazazi wao na hatimaye wazazi hao kumpeleka mtoto katika kituo cha polisi Wilayani Mpanda.
Kwa mjibu wa Bi.Mayorwa mpaka sasa mtoto aliyeokotwa Desemba 1 mwaka huu akiwa hana majeraha wala tatizo lolote la kiafya,yupo katika Hospitali ya Manispaa ya Mpanda kwa uangalizi maalumu na anaendelea na afya njema.
Ametoa wito kwa mama wa mtoto huyo kufika hosptali ya Manispaa ya Mpanda kumchukua ili ampatie malezi yanayostahili.
Tukio hilo linatokea ikiwa ni maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatiri wa kijinsia ambapo kilele chake ni Desemba 10 mwaka huu huku Bi.Redgunda Mayorwa akisema imekuwa mazoe kwa wanawakeMkoani Katavi kutupa watoto.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA