CHADEMA:TAARIFA ZA MNYIKA KUJIVUA UANACHAMA SIYO ZA KWELI ZIPUUZWE
Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema,kimekanusha Mbunge wa Jimbo la Kibamba na mwanachama wa Chadema John
Mnyika kuwa amejivua uanachama.
Mbunge John Mnyika. |
Hatua hii imekuja baada ya taarifa
kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Mbunge huyo amejivua uanachama kwenye
chama chake cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Chama hicho ambacho kimekanusha taarifa
kupitia ukurasa wake wa Twitter kimesema habari hizo hazina ukweli wowote za
zinapaswa kupuuzwa.
Aidha chama
hicho kimesema wanaosambaza habari za Mnyika kujivua uanachama ni walioishiwa
hoja na majibu juu ya maisha ya watanzania.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments