CWT MKOANI KATAVI WAMEANZA KUCHARUKA KUHUSU MADAI YA WALIMU
Na.Issack
Gerald
Chama cha Walimu mkoa wa
katavi CWT kinakusudia kuchukua hatua zaidi kutokana na fedha za walimu manispaa ya Mpanda za makato katika mfuko wa
Jamii PSPF kwa 2008 kutofikishwa.
Hatua hiyo imebainishwa
na Katibu wa chama cha walimu mkoani Katavi Hamisi Chinahova ambapo amesema
suala hilo halijapatiwa ufumbuzi mpaka sasa.
Katika hatua nyingine
amelitaja suala la kukithiri kwa madai mbali mbali ya walimu kuwa kikwazo
katika utendaji kazi ikiwemo kufikia Malengo ya kitaifa.
Mwaka 2015 yaliibuka
madai haya na kupelekea baadhi ya walimu kufanya maandamano ya amani mpaka
ofisi ya mkuu wa mkoa ili kushinikiza malipo ya madeni zikiwemo stahiki mbali
mbali.
Mwezi uliopita Rais
Magufuli alisema madai yote ya watumishi wa umma yangelipwa mwezi uliopita.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments