KAULI YA SERIKALI MANISPAA YA MPANDA IMEWASIKITISHA WATU WENYE ULEMAVU MKOANI KATAVI
Na.Issack Gerald
Watu wenye ulemavu Mkoani
Katavi,wameeleza kusikitishwa na kauli ya serikali kuwa haina pesa za
kuwawezesha kufanya maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani.
Masikitiko hayo wameyatoa leo katika
kikao cha kupanga tarehe nyingine ya maadhimisho ambapo wamepanga yafanyike
Desemba 19 mwaka huu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu SHIVYAWATA Mkoani Katavi Issack
Mlela amesema serikali kutowawezesha kufanya maadhimisho ni kutowatendea haki
wakati serikali inasema mapato yameongezeka serikalini.
Juzi Afisa maendeleo ya jamii
Bi.Marietha Mlozi na Afisa Ustawi wa jamii Bi.Agness Bulaganya wote wa Manispaa
ya Mpanda walikuwa wameiambia Mpanda Radio kuwa maadhimisho ya siku ya Watu wenye
ulemavu yangefanyika Desemba 3 ambayo hata hivyo yameahirishwa baada ya ukosefu
wa pesa.
Haki za watu wenye ulemavu
zinasimamiwa na sheria mbalimbli ikiwemo sheria namba 9 ya mwaka 2010 inayitaka
serikali na jamii kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapatiwa haki katika masuala
yote muhimu hasa katika elimu,afya,kuishi na haki nyingine za kibinadamu ambapo
pia Tanzania ni miongoni mwa taifa katika jumuiya ya madola iliyosaini mikataba
mbalimbali ili kuhakikisha haki za watu wenye ulemavu zinapatikana kama wasio
na ulemavu wanavyohudumiwa ambapo kama nchi haitekelezi haki hizi ni kumnyima
haki mtu mwenye ulemavu.
Maadhimisho ya mwaka huu kitaifa
yamefanyika Mkoani Simiyu na kaulimbiyu ikisema ‘’Badilika kuelekea jamii jumuishi na imara kwa wote’’.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments