RC RUKWA : VIONGOZI WA DINI MUOMBEENI RAIS MAUGUFULI NA WATENDAJI WAKE
Na.Issack
Gerald
MKUU
wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewaomba viongozi wa dini mkoani humo
kuendelea kumuombea rais John Magufuli pamoja na watendaji wengine wa
serikali ili waongoze wananchi kwa kuzingatia misingi ya haki usawa na
kuwaletea maendeleo endelevu.
Wanagabo
ametoa ombi hilo maalumu huo wakati akichangia shilingi milioni moja kwa Baraza
Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa lengo la kusaidia ujenzi wa kituo cha
afya cha Waislamu kinachoendelea kujengwa katika Tarafa ya Kirando Kata ya
Kirando Wilayani Nkasi mkoani humo.
Amesema
rais na watendaji wa serikali ya awamu ya tano wanahitaji kuombewa daima kwani
kufanya kazi ya kuwaongoza wananchi ni jukumu zito linalohitaji msaada wa
Mwenyezi Mungu.
Waka
huo huo amesema taasisi za kidini kwa muda mrefu zimekuwa zikisaidia juhudi za
serikali katika kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia wananchi jambo ambalo pia
linasaidia utekelezaji wa Ilani ya chama tawala inayoongoza serikali.
Ametoa
mchango huo kwa lengo la kuzindua harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa kituo
hicho cha Afya katika siku ya maadhimisho ya mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W)
yaliyofanyika Kimkoa katika Kijiji cha Kabwe Kata ya Kabwe wilayani Nkasi
ambapo alikuwa rasmi katika sherehe hizo.
Kwa upande
wake katibu wa Bakwata mkoani Rukwa Mohammed Khatibu amesema Baraza hilo
linahitaji kiasi cha shilingi 6,910,000 ili kukamilisha ujenzi wa kituo cha
afya ambacho kipo katika hatua ya upauaji.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments