WAENDESHA VYOMBO VYA MOTO WAMETAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA BARABARANI KUELEKEA MWISHONI MWA MWAKA.
Na.Issack
Gerald
Katika
kuelekea siku kuu za mwishoni mwa mwaka
Waendesha vyombo vya moto Mkoani Katavi wametakiwa kuzingatia sheria za usalama
bararani.
Wito
huo umetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoani Katavi Bw.Nassoro
Alfi ambapo amesema madereva wanatakiwa kuwa makini ikiwa pamoja na kufuata
alama za barabarani.
Aidha
mwenyekiti huyo ameuomba uongozi wa manispaa ya Mpanda kuweka vibao vya alama
za usalama barabarani katika manispaa ili kupunguza ajali barabarani.
Katika
hatua nyingine Bw. Alfi amesema Maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani mwaka
2017 kimkoa wa katavi yanatarajiwa
kufanyika kati ya tarehe 17 hadi 20 mwezi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments