WAKAZI WAOMBA TOZO ZA ZIMAMOTO ZISITISHWE MPAKA WAPATE UMEME NA BARABARA IMARA,KAMANDA AJIBU.
Na.Issack
Gerald
Wakazi
wa Kata ya Katumba Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wameliomba jeshi la zimamoto
na uokoaji Mkoani Katavi,kutowatoza tozo za tahadhari ya majanga mpaka wapatiwe
huduma ya umeme na kuboreshewa miundombinu ya barabara.
Wametoa
ombi hilo na kusema kwa sasa hawaoni umuhimu wa kutozwa tozo hiyo,wakati nyumba
zao hazina umeme na barabara hazipitiki kiurahisi.
Kwa
upande wake kamanda wa jeshi hilo Mkoani Katavi Abdallah Maundu amesema,tozo
wanazotoza ni kwa mjibu wa sheria ya nchi na wanatoa huduma katika majanga ya
moto pia katika ajali.
Maeneo
mengi ya Mkoa wa Katavi yana tatizo la miundombinu ya barabara isiyopitika hasa
msimu wa masika,jambo ambalo jeshi la zimamoto na uokoaji linatakiwa kujipanga
namna litakavyotoa huduma kwa wakazi waishio katika maeneo ya miundombinu
mibovu ya barabara.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments