WATOTO WALIOKUWA WAMEPOTELEA MSITUNI MKOANI KATAVI WAMEPATIKANA WAKIWA HAI.
Na.Issack
Gerald
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Katumba Halmashauri
ya wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi,wamekipongeza kituo cha Mpanda Radio kwa
kusaidia juhudi za kupatikana kwa watoto wawili waliokuwa wamepotea katika
mazingira ya kutatanisha.
Wakazi hao wakiwemo Bw.Alex Gezaho,wamesema
siku chache baada ya Mpanda Radio Kutangaza upotevu wa watoto hao wanaojulikana
kwa majina ya Rama na Vitisho walipatikana porini wakiwa na afya njema.
Kwa mjibu wa taarifa zilizokuwa
zimetolewa na viongozi wa Kijiji cha Mnyaki,watoto hao walikuwa wamepotea
wakati wakiwinda ndege porini kwa manati karibu wiki mbili zilizopita.
Kumekuwa na matukio ya upotevu wa
watoto kata ya Katumba ambapo kwa mjibu wa viongozi wa serikali ya Kijiji cha
Mnyaki pamoja na wananchi,mtoto mmoja aliyepotea miaka mitano iliyopita
hakupatikana mpaka sasa hatua ambayo kupatikana kwa watoto Rama na Vitisho
limepokelewa kwa furaha.
Source: Issack
Gerald,Editor:Issack Gerald
Comments