MWENDESHA BODABODA AMEMUUA BODABODA MWENZAKE,ASAKWA NA POLISI PANDE ZOTE
Mwendesha bodaboda maarufu mpaka wa
Sirari na Isebania, Kenya,Kiongera Nchagwa (27) mkazi wa Kijiji cha Gwitiryo,
Tarime Mara anasakwa na Polisi wa pande zote mbili, akituhumiwa kumuua
mwenzake,Jeremia Omera (22) kwa kumchoma kwa kisu kifuani.
Mwenyekiti wa Haki za Binadamu
Wilaya ya Kurya West ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Isebania,
Peter Masaithe amesma tukio hilo limetokana na ugomvi wa kunyang’anyana mizigo
ya abiria aliyetaka kuvuka mpaka kuingia nchini Tanzania akitokea Nairobi Kenya.
Masaithe amekemea bodaboda kutembea
na visu,kunywa pombe za viroba ambavyo baada ya kupigwa marufuku sasa vimehamia
Isebania hali inayochangia uhalifu na kuziomba serikali za nchi hizo mbili
kuchukua hatua kali ukiwemo msako wa viroba na bangi ili kuokoa vijana.
Polisi wa Isebania wamethibitisha
kifo cha Jeremia na wamewasiliana na wenzao wa Sirari kumsaka mtuhumiwa kujibu
tuhuma ambapo pia Polisi wa Sirari wamekiri kupokea taarifa ya mauaji.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Sokoni
Sirari,Benson Makanya amesema waendesha bodaboda Sirari na Isebania wamekuwa
wakitembea na silaha kama visu na kuchangia uhalifu hapo. Mama mlezi wa
Jeremia,mkazi wa Sirari Moraha Roman amesikitishwa na kifo chake na kusema
alikulia kwao.
Ameiomba Serikali imfuatilie
mtuhumiwa kwa madai mara nyingi akifanya matukio hutorokea Mugumu Serengeti kwa
ndugu zake na kurejea baada ya muda.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa
Hospitali ya Ombo Migori ukisubiri ndugu kutoka Soneka Kisii
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments