MATUMIZI YA TOCHI BARABARANI MKOANI KATAVI ZATAJWA KUPUNGUZA AJALI KWA MWAKA 2017
Jeshi la polisi kitengo cha usalama
barabarani mkoani Katavi limesema kuwepo kwa tochi za kudhibiti mwendokasi
kumesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali za barabarani.
Hatua hiyo imebainishwa na Askari wa
kitengo cha Usalama Barabarani John Shindika wakati hali ya usalama katika
kipindi cha mwaka 2017.
Aidha Shindika amewataka watumiaji wa
barabara kuwa makini wawapo barabarani ili kujiepusha na ajali zisizo za lazima.
Katika hatua nyingine Shindika
amesema suala la kuzuia ajali ni wajibu wa kila mtu hivyo kila mmoja yampasa
kuzuia ajali kwa namna yoyote
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments