SERIKALI MKOANI KIGOMA IMETATUA TATIZO LA UHABA WA ARDHI
Jumla
ya Hekta Elfu 10 sawa na hekari 26200
zimepunguzwa kutoka katika hifadhi ya Makere kusini wilayani Kasulu na Kugawiwa
kwa wananchi wa vijiji vya Mvinza na
Kagerankanda.
Hatua
hiyo ni utekelezaji wa agizo la raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John
Magafuli alilolitoa mwezi july mwaka jana wakati wa ziara yake Mkoani Kigoma
lengo likiwa ni kwaongezea wananchi ardhi kwa ajili ya shughuli zakilimo.
Akimwakilisha
Rais,kaimu mkuu wa wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma Kanal Malko Gaguti amesema,mara
baada ya kufanya tathimini katika hifadhi hiyo imeonekana zaidi ya hekta 72
elfu za msitu wa Makere kusini kati ya hizo hekta elfu 18 zimeharibiwa vibaya
kutokana na uvamizi wa shughuli za kilimo.
Wahamiaji
wanoingia nchini kinyume na sheria imeonekana kuwa chanzo kikubwa cha uharibifu
wa misitu lakini pia kufanywa kwa vitendo vya uharifu ambapo Gaguti ambapoa
ametoa rai kwa wakazi wa vijiji Mvinza na Kagerankanda kutumia
vizuri ardhi hiyo
Wakitoa
shukrani kwa serikali kwa niaba ya wananchi kutokana na hatua iliyochukuliwa ya
serikali kutoa eneo hilo kwa wananchi,diwani wa kata ya Kagerankanda Ezeki
Mshingo na Mwenyekiti wa kijiji cha Mvinza Kalos Bukakiye wamesema serikali
imetatua kilio cha wananchi cha muda mrefu ambapo wameahidi kutunza mipaka ya
hifadhi hiyo.
Mwandishi:Isaac Aron Isaac
Mhariri:Issack Gerald
Habari zaidi ni kupitia P5TANZANIA LIMITED
Comments