SUMATRA MKOANI KATAVI YAPONGEZWA KWA KUDHIBITI UPANDISHWAJI NAULI KIHOLELA MSIKUMU WA SIKUKUU
Baadhi ya abiria mkoani Katavi
wameipongeza mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na Nchi kavu (Sumatra)
kwa kusimamia bei za nauli katika msimu wa sikukuu .
Wakizungumza kwa nyakati tofauti
wamesema katika kipindi cha sikukuu mwaka huu bei za nauli hazikupanda
ikilinganishwa na miaka iliyopita
Aidha wamesema kupanda kwa nauli
kunaleta usumbufu kwa abiria ambapo wameiomba Sumatra kuendelea kusimamia swala
la bei za nauli mkoani Katavi.
Tatizo la upandishaji wa nauli
kiholela limeripotiwa kutokea kwa mabasi yaliyokuwa yanafanya safari zake
kutoka Arusha kwenda mikoa mingine katika msimu wa sikukuu hali hiyo
ilisababishwa Sumatra kuingilia kati na abiria kurudishiwa fedha zao huku
mamlaka hiyo ikisema hatua zaidi za kisheria kwa wote waliohusika na
upandishaji nauli.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments