WATU WENYE ULEMAVU MKOANI KATAVI WAMEENDELEA KULIA NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO

Na.Issack Gerald
Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Mkoani Katavi Bw.Issack Mlela amesema Mkoa wa Katavi kushindwa kuwezesha maadhimisho ya watu wenye ulemavu mkoani Katavi ili yafanyike kunawaathiri kwa kuwa kero zao hazisikilizwi.
Bw.Mlela amesema maadhimisho hayo hayakufanyika kwa miaka miwili mfulilizo mwaka 2016 na 2017 akisema baadhi yao kuwezshwa ili kushiriki yanakofanyika kitaifa ilishindikana na hivyo matatizo yao kuendelea kuwaandama bila kupatiwa ufumbuzi.
Aidha Mlela ameiomba serikali kuwashirikisha watu wenye walemavu wanapopanga  bajeti ili kusaidia maadhimisho hayo kufanyika kwa siku maalumu kama inavyokuwa imepangwa kwa ajili ya kuwasilisha kero zao.
Kwa mwaka 2017 serikali ilisema ilishindwa kuwezesha maadhimisho kufanyika Desemba 3 kam yanavyofanyika kila mwaka kimataifa kutokana na ukosefu wa fedha huku hata tarehe nyingine ya Desemba 19 iliyokuwa imepangwa kuadhimishwa siku ya watu wenye ulemavu duniani ikiahirishwa pia kutokana na ukosefu wa pesa.
Wakati huo huo Mlela ametoa wito kwa wakazi wa mkoani Katavi kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanapatiwa elimu kwa ajili ya maisha ya baadaye.
Amesema baadhi ya watoto wameendelea kukosa elimu kama haki yao ya msingi kutokana na jamii kuendelea kuwaficha majumbani.
Katika Mkoa wa Katavi kuna watu wenye ulemavu mbalimbali zaidi ya 2000 wakiwa wamegawanyika katika ulemavu wa wasioona,viziwi,viungo,ualbino na usonji.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED




Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA