JAMII WILAYANI MPANDA IMETAKIWA KUWAJALI WATU WENYE MAHITAJI MAALUMU
Na.Issack Gerald
Jamii mkoani katavi imetakiwa
kuwajali watu wenye mahitaji maalumu ili kuwawezesha kushiriki katika shughuli
mbalimbali za uzalishaji mali
Wito huo umetolewa na Afisa ustawi wa
jamii wa Manispaa ya Mpanda Bi.Agness Bulaganya ambapo amesema idara ya ustawi
wa jamii inaendelea kutoa elimu shirikishi ili kuhakikisha jamii inapata uelewa
wa kuishi na watu walio katika makundi hayo.
Katika hatua nyingine Bi.Buraganya
amesma endapo jamii inakuwa na mwamko wa kuwatambua watu walio kwenye makundi
hayo,serikali mkoani Katavi iko tayari kuyaunganisha na fursa mbalimbali
zitakazowawezesha kuijtegemea
Amesema kwa mwaka wa 2018 idara ya ustawi
wa jamii mkoani Katavi imejipanga kushughulikia masuala mbalimbali ikiwemo
kupunguza ongezeko la mimba za utotoni.
Kauli ya serikali kuhusu watu wenye
mahitaji maalumu inakuja ikiwa ni siku moja baada ya shirikisho la vyama vya
watu wenye ulemavu mkoani Katavi kusema kuwa serikali ya awamu ya tano
haiwajali katika mahitaji yao kama inavyostahili hasa katika kusikiliza kero
zao ikiwemo kuadhimisha siku maalumu zinazohusu makundi hayo ili wapate nafasi
ya kueleza kero zao.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments