ABUBAKAR SHEKAU AIBUKA TENA NA UJUMBE NCHINI NIGERIA
Kiongozi wa kikundi cha wapiganaji wa Boko Haram
Abubakar Shekau,ameonekana kwenye video mpya karibu saa ishirini na nne baada
ya Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kwa mara nyingine kutamka hadharani kuwa
kikundi hicho kimesambaratishwa.
Huu
ni mkanda wa video wa kwanza kutolewa na Shekau baada ya kimya cha miezi kadhaa
iliyopita huku akiwa ni mongoni mwa viongozi wanaosakwa kwa baada ya kupewa sifa
ya kuwa miongoni mwa magaidi wanaosakwa na Marekani pamoja na mamlaka ya
Nigeria.
Abubakar
Shekau anaonekana kwenye mkanda huo wa video akiwa ameketi peke yake akiwa
amevalia kanzu,kofia yenye rangi inayofanana na bunduki aina ya AK-47 ambayo
anaonekana kuwa na mahaba nayo Lakini anaonekana kushindwa kuzungumza kwa sauti
yenye mamlaka ikilinganishwa na matamko yake ya awali .
Akisoma
kutoka katika karatasi kwa lugha ya kiarabu na ki Hausa,Shekau,anakiri kundi
lake kuhusika katika matukio ya hivi karibuni nchini Nigeria katika maeneo ya
kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo ikiwemo lile lililotukia siku ya siku kuu ya
Christimas katika kijiji cha Molai nje ya jiji la Maiduguri,mji mkuu wa Jimbo
la Borno.
Shekau
alijinasibu kwa kusema askari wa kundi la wanamgambo la Boko Haram wana afya njema
na kwamba vikosi vya ulinzi nchini Nigeria haviwezi kufanya lolote dhidi ya
wanamgambo wake.
Sehemu
ya dakika thelathini na moja ya mkanda huo zimeoneshwa mbwembwe za wapiganaji
wa kundi hilo ikiwemo magari ya silaha,malori na pikipiki huku wakipiga risasi
hewani kwa kile kinachoonekana kizuizi cha njiani katika kambi ya kijeshi
iliyotelekezwa .
Wakati
huo huo Shekau alionekana akitoa tamko juu ya kukerwa kwake dhahiri juu ya
kutambuliwa hivi karibuni mji wa Yerusalemu kama mji mkuu wa Israeli tamko
lililotolewa na Rais wa Marekani Donald Trump.
Abubakar Shekau,ameijosoa nchi ya Saudi
Arabia kwa kushirikiana na wale aliowaita makafiri na kuwalaumu Wapalestini kwa
uharibifu wao.
Mpaka
sasa serikali ya Nigeria haijatoa tamko lolote juu ya mkanda huo wa video na
ujumbe uliomo ndani yake huku jeshi la Nigeria likikiri kuwafukuza waasi kutoka
katika ngome zao kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo.
Hata hivyo hivyo wanamgambo wa kikundi
cha wapinaji cha Boko Haram bado wanaendeleza mashambulizi ya kujitoa muhanga,mashambulizi
ya risasi za moto zaidi wakilenga vifaa vya kijeshi na vijiji.
Habari
zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments