RAIS MAGUFULI AMTEUA MNADHIMU WA JWTZ APANDISHA VYEO MABRIGEDIA 10 KUWA MAJENERALI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe.Dkt.John Pombe
Magufuli leo amemteua Meja Jenerali Yakubu Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Rais wa Tanzania Mh.Dkt John Pombe Magufuli |
Pamoja
na uteuzi huo,Mhe.Rais Magufuli amempandisha cheo kutoka Meja Jenerali na kuwa
Luteni Jenerali.
Kwa
mjibu wa taarifa ambayo imetolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa
Mawasiliano ya Rais ikulu ya Rais,Gerson Msigwa Luteni Jenerali Yakubu Hassan
Mohamed anachukua nafasi ya Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwa ambaye
amestaafu.
Aidha,Mhe.Rais
Magufuli amewapandisha vyeo kutoka Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenerali
wafuatao;
1.
Brig Jen. J.G. Kingu
2.
Brig Jen. M.S. Busungu
3.
Brig Jen. R.R. Mrangira
4.
Brig Jen. B.K. Masanja
5.
Brig Jen. G.T. Msongole
6.
Brig Jen. A.F. Kapinga
7.
Brig Jen. K.P. Njelekela
8.
Brig Jen. A.S. Bahati
9.
Brig Jen. M.E. Mkingule
10.
Brig Jen. S.S. Makona
Mabrigedia
Jenerali wote waliopandishwa vyeo watapangiwa vituo vya kazi baadaye huku Mnadhimu
Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed akitarajiwa kuapishwa kesho 15
Februari 15 kuanzia saa saa 5:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Habari
zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments