FAHAMU ASILI NA MAANA HALISI YA SIKU YA WAPENDANAO’’VALENTINE DAY’’
Siku ya Valentines Day asili yake ni kutoka
Dola ya Warumi.
Ni siku ya kumbukumbu (memoria day) na sehemu
nyingine ni (festum) maana yake siku kuu ya daraja la kwanza kwa kumkumbuka
Padre Valentine aliyeuawa na utawala wa kirumi kwa Sababu ya kutetea waumini
wake kufunga ndoa badala ya kuishi na vimada tu.
Lakini sikukuu hiyo imeenea sana katika nchi za
magharibi na baadaye karibu sehemu kubwa ya ulimwengu kuisherehekea kama siku
yamapenzi kinyume cha dhamira ya Mt.Valentine.
Watawala wa dola ya kirumi walikuwa na fikra za
kueneza dola ya kirumi duniani kote na hivyo vijana hawakutakiwa kuoa,ili wawe
huru muda wote kwenda vitani kupigania nchi kwa sababu kwamba wakioa wasingekuwa
na uhuru wa kwenda vitani bali kuwa na famiia zao.
Vijana wengi wakawa na mtindo wa kuwa na vimada
tu kitu ambacho kanisa lilikukwa linapinga.
Padre Valentine ambaye alikuwa Roma akawa
anawahimiza vijana kufunga ndoa badala ya kufanya ngono bila ndoa kwani ni
dhambi na kitu kisichokubalika mbele ya Mungu.
Akawa anafungisha ndoa kwa siri kwenye
makatakombe (mahandaki chini ya kanisa ambako kuna sehemu za ibada kwa watu
wachache),alifanya hivyo kwa vile kufunga ndoa hadharani ilikuwa ni kukiuka
amri ya wakuu wa dola ya kirumi.
Baadhi ya watu walifichua siri hiyo,hivyo Padre
Valentin alishikwa na dola ya Warumi na kuuawa kama shahidi mfia dini kwa ajili
ya kutetea waamini wake wafunge ndoa badala ya maisha ya ngono zembe bila ndoa.
Wakristo wakawa siku ya kumkumbuka Padre
Valentin kama mfia dini sababu ya kutetea maisha ya wanakanisa kuwa wanandoa,Ikaenea
katika kanisa nchi za magharibi na hata duniani ambako wanakanisa wanamkumbuka
Mt. Padre Valentin.
Baadaye ikapokeleka na watu hata wasio na
imani ya kikristo kama ni siku ya kufanya kumbukumbu kwa Mt. Valentin kama
mtetezi wa Ndoa.
Maudhui ya siku hiyo kwa wasiowanakanisa
imechukua maana nyingine ya kwamba ni siku ya wapendanao hata kwa wasio wanandoa
bali mradi wanapendana,kitu ambacho ni kinyume cha malengo ya mfia dini Mt.Padre
Valentin aliyetaka vijana wafunge ndoa badala ya kuwa na hawara tu (vimada).
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments