DC ACHARUKA WANANCHI KUTAPELIWA FEDHA ZA MASHINE ZA EFDs
SERIKALI mkoani Katavi imetoa siku 14
kwa makampuni na wafanyabiashara waliochukua fedha kwa ajili ya kuwauzia
mashine za EFDs wafanyabishara na mpaka sasa hawajui hatma ya fedha zao.
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Lllian Matinga alitoa siku hizo jana katika kikao maalumu cha kusikiliza kero za
wafanyabiashara wa mkoa huo akimwakilisha mkuu wa mkoa huo Meja jenerali Mstaafu
Raphae Muhuga.
Alisema amefikia uamuzi huo baada ya
kuwepo kwa makampuni yaliyokusanya fedha kutoka kwa wafanyabiashara na kuahidi
kuwapelekea mashine za EFDs lakini mpaka sasa hawajapatiwa mashine hizo.
Matinga alisema kutokana na kuwa
wafanyabiashara hao hawajui hatma ya fedha zao na mpaka sasa hawajapata mashine
hizo hivyo ameamua kutoa siku hizo warudishiwe fedha zao vinginevyo hatua za
kisheria zitachukuliwa.
Awali katika kikao hicho mwenyekiti
wa wafanyabiashara wa mkoa huo Hasanaal
Dalla alimwambia mkuu huyo wa wilaya kuwa wafanyabiashara wa mkoa huo
wametapeliwa na makampuni ambapo yamechukua fedha zao kwa ahadi kuwa watawaletea
mashine za EFDs lakini imekuwa ni tofauti.
Alisema imepita muda mrefu mpaka hivi
sasa ambapo fedha za wafanyabiashara zimechukuliwa na hawajui hatma yao ni nini
hivyo alimuomba mkuu huyo wa wilaya awasaidie.
Mwenyekiti huyo alisema baadhi ya
wafanyabiashara wanaonekana hawatii agizo la serikali la kuwataka watumie
mashine hizo lakini ukweli ni kwamba walikwisha lipa fedha ili wapate mashine
hizo lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea.
Hata hivyo Mkuu wa wilaya huyo mwaka
jana alitoa agizo kama hilo kwa makampuni na wafanyabiasahara hao lakini haijajulikana
kama agizo lake lilitekelezwa.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments