WANAFUNZI WANYESHEWA MVUA WAKISOMEA CHINI YA MIEMBE WILAYANI MPANDA,WAZAZI WAISHIWA NGUVU WAIOMBA SERIKALI KUSAIDIA
Na.Issack Gerald-Mpanda
Wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika
Shule ya Msingi Sambwe iliyopo mtaa wa Kampuni Kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda,wameiomba
serikali kuwasaidia kumalizia ujenzi wa madarasa katika shule hiyo ili
wanafunzi hao waondokane na adhaa ya kunyeshewa na mvua inayoambatana na radi wakiwa chini ya miembe.
Moja ya mwembe unaotumiwa na wanafunzi kama darasa ukitumika kama ukumbi wa mikutano ya wazazi Shule ya msingi Sambwe |
Hayo yamebainishwa na wazazi hao
wakati wakizungumza na P5 TANZANIA MEDIA
Sambamba na Mpanda Radio Katika mtaa huo,kuhusu namna wazazi wanavyojitolea
katika ujenzi wa madarasa shuleni hapo.
Aidha wamesema kuwa,baadhi ya watoto
wamekuwa wakiugua magonjwa kama homa,maralia na mengineyo huku daftari
zikilowana kutokana na wanafunzi kukosa mahala pa kujisitiri.
Baadhi ya Wazazi waliozungumza ni
pamoja na Mussa Daudi,Huruma Washega na Peter Paul Masesela wote wakazi wa Mtaa
wa Kmpuni ambao pia wamesema kutokana na kuishiwa pesa hawana namna zaidi ya
kuitegemea serikali kutokana na uwezo wao kufikia kikomo.
Hata hivyo wameeleza kusikitishwa na
serikali kuwafukuza wachimbaji wadogowadogo katika mgodi wa Kampuni ambapo
wachimbaji hao kila mara wamekuwa sehemu mojawapo ya chanzo cha Mapato katika
kuendesha maendeleo ya shule.
Katika hatua nyingine,wameiomba
serikali kumuweka katika mfumo wa malipo
mwalimu Alex Sangu ambaye amekuwa akifundisha katika shule ya Sambwe kwa muda
mrefu ikizingatiwa kuwa hawana tena uwezo wa kulipa kutokana na kipato chao
kidogo kinachotosheleza kuendesha familia zao.
Hata hivyo Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo
Bw.Charles Kassian ,hakuwa tayari kuzungumza na P5 TANZANIA MEDIA sambamba na Mpanda
Radio kuhusu maendeleo na hali ya shule zaidi ya kusema kuwa labda atazungumza baada
ya mwezi mmoja kuanzia sasa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa
Kampuni Bw.James Simon amekiri wanafunzi kusomea chini ya miembe tangu shule
zifunguliwe Januari 11 mwaka huu
ukizingatia kuwa ni msimu wa mvua za masika zinazoambatana na radi.
Hata hivyo Bw.Simoni,amewataka
wananchi kuendelea kuwa wavumilivu wakati masuala mbalimbali yakiwemo kumlipa mwalimu
wakati yakifanyiwa kazi ambapo wakati huo huo amesema kuwa siku ya jumatano ya
wiki ijayo wanatarajia kuitisha mkutano wa hadhara kujadili maendeleo ya shule.
Shule ya Msingi Sambwe,ina walimu 2
walioajiriwa na seriklai huku mmoja akiwa ni wa kujitolea ambo shule hiyo iliyosajiriwa
mwaka huu ina wanafunzi wapatao 150 kuanzia darasa la kwanza hadi la nne.
Hata hivyo Meya wa Manispaa ya Mpanda Bw. Philipo Mbogo ambaye ni miongoni mwa walioanzisha shule hiyo baada ya kuona kuwa watoto wanahangaika kwenda kusomea umbali mrefu,ameiambia P5 TANZANIA MEDIA na Mpanda Radio Kuwa suala la shule hii linafahamika na linafanyiwa kazi.
Siku ya jana,kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari,alitoa wito kwa wakazi Mkoani Katavi kujikinga na mvua sehemu iliyo salama ikiwa ni pamoja na kueupa kwenda chini ya miti ambapokwa kiasi wanafunzi hawa hawatofauriani na mazingira kama hayo kwa kuwa hakuna madarasa.
Hata hivyo Meya wa Manispaa ya Mpanda Bw. Philipo Mbogo ambaye ni miongoni mwa walioanzisha shule hiyo baada ya kuona kuwa watoto wanahangaika kwenda kusomea umbali mrefu,ameiambia P5 TANZANIA MEDIA na Mpanda Radio Kuwa suala la shule hii linafahamika na linafanyiwa kazi.
Siku ya jana,kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari,alitoa wito kwa wakazi Mkoani Katavi kujikinga na mvua sehemu iliyo salama ikiwa ni pamoja na kueupa kwenda chini ya miti ambapokwa kiasi wanafunzi hawa hawatofauriani na mazingira kama hayo kwa kuwa hakuna madarasa.
Mshirikishe na mwezio Kuhusu P5 TANZANIA MEDIA
Comments