TAMISEMI YAAGIZWA KUSIMAMIA VIZURI HALMASHAURI
Na.Issack Gerald-Katavi
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) ndiyo kitovu cha nchi na kwamba kila Mtanzania ameelekeza jicho lake
pale kwa sababu anasubiri kupata huduma ya msingi.
Ametoa
kauli hiyo leo wakati akizungumza na wakurugenzi, wakuu wa taasisi na watumishi
wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwenye mkutano uliofanyika ofisi ya TAMISEMI mjini
Dodoma.
Waziri
Mkuu ameitaka ofisi hiyo ihakikishe inaisimamia vizuri mikoa na halmashauri ili
Serikali iweze kupata matokeo mazuri na tarajiwa.
Waziri
Mkuu alisema jukumu kubwa lililopo hivi sasa katika Mamlaka za Serikali za
Mitaa ni kuhakikisha kuwa zinabuni vyanzo vipya vya mapato na kusimamia vizuri
ukusanyaji wa mapato ya serikali.
Alisema
Serikali ya Awamu ya Tano imekusudia kuwahudumia ipasavyo Watanzania wenye
uelewa tofauti na matakwa tofauti na kwa kuanzia Serikali imeanza kuwajenga
watumishi wa Serikali kutambua kuwa wao ni wahudumu wa wananchi hivyo inawapasa
kuwahudumia vema.
Awali akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na watumishi hao,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Bw. George Simbachawene alisema
TAMISEMI wapo tayari kubadilika na kufanya kazi kama kauli ya Rais John Pombe
Magufuli inavyotaka, yaani HAPA KAZI TU.
Naye,
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Bernard Makali alimpongeza Waziri Mkuu
Majaliwa kwa kusimamia vizuri masuala ya elimu nchini wakati akiwa Naibu Waziri
wa TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya elimu.
Chanzo
cha Habari : Ofisi ya Waziri Mkuu
Comments