MAAFISA ELIMU NSIMBO WAPEWA SIKU 6 KUHAKIKISHA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUINGIA SEKONDARI WANARIPOTI
Na.Agness Mnubi-Nsimbo.
MAAFISA
elimu sekondari katika halmashauri ya wilaya ya Nsimbo wamepewa siku 6 kuanzia
jana, kuhakikisha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha
kwanza wanaripoti.
Akizungumza
juzi katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo, Mkuu
wa Wilaya ya Mlele kanali mstaafu Issa Suleiman Njiku, amesema mahudhurio ya
wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza si mazuri na
kuwataka maafisa elimu kushirikiana na wenyeviti na watendaji wa vitongoji,
vijiji na kata, kuhakikisha wanafunzi hao wanaripoti shuleni.
Aidha
Kanali Njiku ameutaka uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo kuhakikisha
unatekeleza tamko la Waziri wa TAMISEMI juu ya kutatua changamoto ya upungufu
wa madawati.
Amesema
mkoa wa Katavi umetoa muda hadi mwisho
wa mwezi Machi, kuhakikisha halmashauri zote zinatekeleza agizo hilo, na halmashauri
ambayo haitatekeza, Mkurugenzi atachukuliwa hatua za kisheria.
Comments