JAMII NSIMBO YAOMBWA KUSHIRIKI MATENGENEZO YA MIUNDOMBINU YA BARABARA
Na.Vumilia Abel-Nsimbo
JAMII
wilayani Nsimbo mkoani katavi imeombwa kushiriki katika matengenezo madogo madogo
ya miundombinu ya barabara.
Ushauri
huo umetolewa na mkurugenzi wa
halmashauri ya Nsimbo Bw Michael Nzyungu wakati akizungumza na P5 TANZANIA sambamba na mpanda radio Ofisini kwake.
Amesema,
hali ya
miundombinu ya barabara hairidhishi
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha
na kuwa baadhi hazikusajiliwa wala kutengewa bajeti, na zipo katika
mikakati ya kusajiliwa ili zipatiwe bajeti kwa mwaka wa fedha 2016 /2017.
Bw.
Nzyungu amezitaja baadhi ya barabara zilizotengewa bajeti ni
Itenka, Magamba, Kasalala, Sungamila, Katumba complex1 na Katumba complex B, Urwila na Usense.
Aidha,
amewataka madiwani na watendaji waonapo
dalili hatarishi ya kuharibika miundombimu hiyo watoe taarifa mapema ili hatua zichukuliwe.
Comments