MKOA WA KATAVI KUTOA SEMINA KWA VIONGOZI WA NGAZI ZA MITAA ILI KUTAMBUA MAJUKUMU YAO
Na.Boniface Mpagape:Mpanda
SERIKALI
Mkoani katavi inatarajia kutoa semina kwa viongozi wa serikali kuanzia ngazi za
vijiji, kata na tarafa ili watambue vyema majukumu yao.
Mkuu
wa mkoa wa katavi Dk. Ibrahim Msengi amesema hayo wakati akizungumza na P5
TANZANIA MEDIA Sambamba na Mpanda radio ofisini kwake. Amesema imebainika kuwa
baadhi ya viongozi wa serikali katika ngazi hizo mkoani Katavi wamekuwa
hawatambui vizuri majukumu na mipaka ya madaraka waliyonayo.
Amesema
semina hiyo inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni itawajengea uwezo wa kutambua
uwajibikaji wao kwa wananchi na kurahisisha utendaji kazi.
Aidha
Mkuu wa mkoa wa Katavi amesema semina hiyo itakuwa ni chachu ya kuleta
mabadiliko katika ngazi za uongozi kwani wahusika watapaswa kutoa taarifa
kuhusu utendaji wao na itakuwa rahisi kupima uwajibikaji wao katika shughuli za
maendeleo.
Comments