HAYA MAMBO YA USALAMA WA TANZANIA NA WATU WAKE YANAHITAJI ZAIDI YA TAFAKARI
Mwenyekiti
wa Chadema,Freeman Mbowe amesema gharama za matibabu ya Mbunge wa Singida
Mashariki, Tundu Lissu aliyelazwa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya
zimefikia Sh412.7 milioni.
Lissu
ambaye ni mwanasheria wa chama hicho, amelazwa hospitalini hapo tangu Septemba
7 aliposhambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi akiwa maeneo ya nyumbani kwake Area
D mjini Dodoma.
Mbowe
akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne, Oktoba 17, 2017 jijini Dar es
Salaam, Tanzania amesema gharama ni kubwa, ila anawaomba Watanzania wasichoke
kuchangia kwa kuwa Lissu atarudi barabarani.
Kuhusu
mchanganuo wa michango, Mbowe amesema wabunge wa Chadema wamechanga Sh48.4
milioni.
Amesema
wananchi wamechangia Sh24.2 milioni kupitia simu ya Mbunge wa Tarime Mjini
(Chadema), Esther Matiko.
Mbowe
amesema wabunge wote wakiwemo wa Chadema wamechanga Sh43 milioni na kwamba,
Watanzania walio nje ya nchi wamechanga kupitia Go fund me Dola 29,000 za
Marekani.
Kiongozi
huyo wa Chadema amemshukuru Mange Kimambi kwa kufanya kazi kubwa ya kuhamasisha
michango.
Mbowe
amesema wafanyabiashara wakihamasishwa na Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema),Godbless
Lema wamechanga Dola 18,000.
Amesema
wana orodha nzima ya wote waliochangia na amewaomba Watanzania waendelee
kuwapigania.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments