WATU WA TUME YA UCHAGUZI NCHINI KENYA WAANZA KUNG’ATUKA MADARAKANI
Dkt Akombe ametuma taarifa kutoka mjini New York anakoishi
ambapo alikuwa akiufanyia kazi Umoja wa Mataifa kabla ya kujiunga na tume ya
IEBC.
Katika taarifa, Dkt Akombe alisema kuwa merejeleo ya uchaguzi
utakaofanyika hayaafikii matarajio ya uchaguzi ulio huru na wa haki.
Dkt Akombe alitarajiwa kuwa miongoni mwa kundi la maafisa
waliokwenda Dubai kuchunguza uchapishaji wa makaratasi ya kupigia kura.
Dkt Akombe alizuru Nyanza na maeneo ya Magharibi, ambayo ni
ngome ya upinzani, wiki iliopita huku tume hiyo ikijaribu kuwafunza maafisa
watakaosimamia uchaguzi huo.
Comments