FAHAMU MAISHA YA DKT ROSELYN WA TUME YA UCHAGUZI ALIYEJIUDHURU NCHINI KENYA

Dkt Roselyn Akombe Kwamboka alizaliwa 1976 katika kaunti ya Nyamira , na kusomea katika chuo kikuu cha Nairobi kabla ya kuelekea nchini Marekani kwa masomo zaidi.
Anamiliki shahada ya uzamifu katika maswala ya sayansi na kimataifa mbali na shahada nyengine kama hiyo katika somo hilo kutoka chuo kikuu cha Rutgers .
Hadi uteuzi wake katika tume hiyo alifanya kazi kama katibu katika Umoja wa Mataifa mjini New York, wadhfa ambao anasema ulimwezesha kuwa na uzoefu katika maswala ya uchaguzi duniani.
Uwezo wake mkuu alisema mbele ya kamati ya bunge nchini Kenya , ni kutatua migogoro na kwamba ameishi ng'ambo kwa takriban miaka 15, hatua iliomwezesha kuelewa zaidi mahitaji ya watu wanaoshi ughaibuni wakati wa uchaguzi.
Kwamboka alielezea kwamba alichukua uamuzi huo kama Mkenya mzalendo aliyetaka kulihudumia taifa lake.
Alichukua likizo katika Umoja wa Mataifa hatua inayomaanisha kwamba hatopokea hata shilingi kutoka Umoja wa mataifa wakati ambapo amekuwa akiifanyia kazi IEBC.
Yeye pia anaamini kwamba lazima kuwe na mfumo unaounganisha orodha ya wapiga kura na sajili ya watu , na kwamba Wakenya pia wanahitaji kuhamasishwa kuhusu elimu ya uchaguzi.
Hatahivyo anaamini kwamba kila mshikadau ana jukumu la kuhakikisha kuwa viwango vya joto la kisiasa havisababishi ghasia.


Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au ukurasa P5Tanzania Limited

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA