MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI KENYA AMEWALAUMU WANASIASA
Bw
Chebukati amesema maandalizi ya uchaguzi huo yanaendelea vyema lakini katika
mazingira ya sasa ni vigumu kuandaa uchaguzi huru na wa haki iwapo hakutakuwa
na mabadiliko.
Amesema
pia kwamba maafisa wakuu kwenye tume ya uchaguzi ambao wametajwa kwa njia moja
au nyingine kwamba walihusika katika kuvuruga uchaguzi wa kwanza tarehe 8
Agosti wanafaa kujiuzulu.
Bw
Chebukati amesema hayo saa chache baada ya mmoja wa makamishna wa wa tume hiyo
Dkt Roselyn Akombe kutangaza kujiuzulu akiwa Marekani na kusema hana mipango
yoyote ya kurejea Kenya hivi karibuni.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
IEBC ilimtangaza Rais Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika tarehe 8
Agosti, akiwa mbele ya mpinzani wake Raila Odinga wa muungano wa upinzani Nasa
kwa zaidi ya kura 1.4 milioni.
Bw Odinga
alipinga matokeo hayo mahakamani na Mahakama Kuu ikaamua ulijaa kasoro nyingi
na kuagiza uchaguzi mpya ufanyike katika kipindi cha siku sitini.
Tume ya
uchaguzi ilitangaza tarehe mpya ya uchaguzi kuwa 26 Oktoba lakini Bw Odinga
alijiondoa wiki iliyopita akisema mageuzi ambayo yalifaa kutekelezwa
kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki hayajatekelezwa.
Comments