MADIWANI WANAOTUHUMIWA KUNUNULIWA NA CCM WAHOJIWA NA TAKUKURU
Maofisa
wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kutoka makao makuu
jijini Dar es Salaam, wamewahoji kwa zaidi ya saa sita,madiwani waliojiuzulu
Chadema wanaotuhumiwa na Mbunge wa Arumeru Mashariki,Joshua Nassari kuwa
walipewa rushwa.
Waliofika
Takukuru ni Catherine Mtui,aliyekuwa diwani wa viti maalumu,Japhet Jackson(aliyekuwa
diwani wa Ambuleni) na Bryson Isangya (aliyekuwa diwani wa Maroroni).
Baada
ya kuhojiwa hawakutaka kuzungumza chochote wakisema wanaacha uchunguzi
uendelee.
Pamoja
nao, diwani wa Mbuguni,Ahimidiwe Rico anayedaiwa kuwa ndiye alirekodi sauti na
picha wakati akishawishiwa na viongozi wa Serikali na wa Halmashauri ya Meru
amehojiwa kwa zaidi ya saa tatu jana Jumanne Oktoba 17, 2017.
Rico
amesema amewaeleza Takukuru kila kitu ambacho anakifahamu katika sakata hilo,
ikiwemo kuwarekodi viongozi ambao walimshawishi kujiuzuru udiwani.
Rico
aliyesindikizwa na diwani wa Nkwanankore, Wilson Nanyaro amesema
ana imani na Takukuru kwamba watafanya uchunguzi wa kina na kuchukua hatua.
Alisema
baada ya mahojiano yaliyoanza saa tatu hadi saa sita mchana, maofisa wa
Takukuru walimwambia aondoke na watamuita watakapomuhitaji.
Hakuna
ofisa wa Takukuru aliyekuwa tayari kuzungumzia mahojiano hao wakisema wasemaji
ni makao makuu ya ofisi hiyo Dar yaliyoko jijini Dar es Salaam.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited
Comments