SEKTA YA UCHIMBAJI MADINI MKOANI KATAVI,VIJANA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA
Vijana mkoani Katavi wametakiwa kutumia fursa
ya machimbo ya madini ya dhahabu yaliyopo mkoani Katavi katika kujiinua
kiuchumi.
Hayo yamesemwa na baadhi ya wachimbaji wadogo
wadogo wanaofanya shughuli hiyo katika machimbo ya dhahabu yaliyopo katika
kijiji cha Dirifu Mjini Mpanda.
Katika hatua nyingine wachimbaji hao wamewataka
vijana kupuuza maneno ya baadhi ya watu kuhusiana na kazi ya uchimbaji madini
kwani migodini kuna shughuli mbalimbali ambazo hazihatarishi maisha ya wachimbaji.
Licha ya
sehemu nyingi za wachimbaji wadogo wadogo kutokuwa rasmi, uchimbaji wa madini
ni moja kati ya sekta iliyoajiri vijana wengi mkoani Katavi
Habari
zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au
ukurasa P5Tanzania Limited
Comments