WATU WENYE ULEMAVU MKOANI KATAVI KESHO KUPATIWA ELIMU YA KUJIKWAMUA KIUCHUMI
Na.Issack
Gerald-Katavi
IDARA ya maendeleo ya ustawi wa jamii Manispaa
ya Mpanda Mkoani Katavi,kesho inatarajia kuendesha semina kwa watu wenye
ulemavu ili kuwapatia elimu ya namna ya kujikwamua na umaskini kwa kufanya
shughuli za maendeleo.
Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya watu
wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Mkoani Katavi Bw.Issack Lucas Mlela
amethibitisha hatua hiyo ya Halmashauri kuleta semina hiyo kwao na kusema
semina hiyo itakuwa mwanga kwao kufanya shughuli za maendeleo zenye tija.
Mwezi
uliopita,Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Mkoani Katavi lilisikika
likilalamika kusahaulika kwa watu wenye ulemavu katika fursa za maendeleo
hususani katika ugawaji wa mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali kutoka idara za
maendeleo ya jamii.
Mkoa Wa
katavi unakadriwa kuwa na watu wenye ulemavu zaidi ya 2000 huku wakigawanyika
katika makundi ya watu wasioona,wenye usonji,ulemavu wa ngozi albino,ulemavu wa
viungo,kutosikia(viziwi) na wenye mtindio wa ubongo.
Comments