WAKURUGENZI MANISPAA YA SUMBAWANGA KIKAANGONI FEDHA ZA WAKANDARASI
WAKURUGENZI
wa halmashauri ya wilayani ya Sumbawanga na Manispaa mkoani Rukwa wameingia
matatani kwa kitendo cha kuhamisha fedha za malipo ya wakandarasi na kuzipeleka
kutengeneza madawati.
Akizungumza
katika kikao cha Bodi ya barabara yamkoa huo mwenyekiti wa wakandarasi
Anyosisye Kiluswa alisema kuwa fedha hizo kiasi cha shilingi milioni 250
wamekuwa wakizidai kwa muda mrefu pasipo mafanikio.
Alisema kuwa wakandarasi wa ndani wanadai fedha hizo tangu mwaka
2016 baada ya kukamilisha miradi ya maji,barabara, na ujenzi wa vyumba vya
madarasa ambazo hawajalipwa kwa muda mrefu.
Kiluswa alisema kuwa fedha hizo zilikuwa ni za matazamio baada
ya kukamilika kwa mradi ambazo zinapaswa kulipwa ndani ya kipindi cha miezi
mitatu mpaka sita tangu kukamilika kwa mradi lakini ni zaidi ya mwaka na nusu
hawajalipwa.
Alisema walipo kuwa wanatekeleza miradi hiyo fedha hizo
zilikuwepo lakini watendaji wa halmashauri walibadili matumizi na kuzielekeza
kwenye kutengenezea madawati kitendo kilicho sababisha wasilipwe mpaka sasa.
Mwenyekiti huyo wa wakandarasi alisema kuwa hivi sasa baadhi ya
wakandarasi wanakabiliwa na madeni kwani baadhi yao walikopa fedha katika
mabenki,huenda mali walizo weka dhamana zikapigwa bei na hivyo kujikuta
halmashauri zimewasababishia umasikini wa kutupa.
Hata hivyo gazeti hili lilipo mtafuta mkurugenzi wa Manispaa ya
Sumbawanga Hamid Njovu ili kupata ufafanuzi wa madai hayo alisema kuwa
halmashauri yake haidaiwi na mkandarasi yoyote kwani mpaka Tarula inaanzishwa
halmashauri hiyo ilikuwa na fedha kiasi cha shilingi milioni 360 na angeweza
kulipa.
Naye mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga John
Msemakweli alisema kuwa baada ya kuanzishwa TARULA waliikabidhi kazi zote
pamoja na madeni ya wakandarasi ndio wanapaswa kuyalipa.
Akizungumzia malalamiko hayo katika kikao cha bodi ya
barabara ya mkoa katibu tawala mkoa wa Rukwa Bernard Makali alisema kuwa
ataziandikia barua halmashauri hizo na TARULA wahakikishe wanalipa madeni hayo
haraka iwezekanavyo kwani yamekuwa ni ya muda marefu.
Habari
zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com au
ukurasa P5Tanzania Limited
Comments