JESHI LA POLISI MKOA KATAVI LIMESEMA LIMEJIPANGA KUDHIBITI UHARIFU KATIKA VIPINDI VYA SIKUKUU

Na.Issack Gerald
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda amewataka wananchi kusherekea kwa amani Sikukuu zinazokaribia kwa kufuata sheria zilizowekwa.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati akizungumzia namna ambavyo jeshi la polisi Mkoani Katavi limejipanga ili kuhakikisha wananchi wanasherehekea kwa amani bila kuwepo na uvunjifu wa amani.
Kamanda Damas Nyanda
Aidha amewataka wazazi kuwa makini na watoto wao hasa katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu na kutoa ovyo kuwa watoto hawaruhusiwi kuingia maeneo ya disco.

Jeshi la polisi mara kwa mara limekuwa likisema wananchi wamekuwa hawaripoti baadhi ya viashiria vya matukio ya uharifu ambayo baadaye yamekuwa yakisababisha madhara ambapo amewataka kuripoti viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani ili hatua za udhibiti zichukuliwe haraka.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA