SOKO LA HALMSHAURI YA WILAYA YA NSIMBO NI CHAFU HALINA CHOO TANGU MWAKA 1975
Na.Issack Gerald
Soko la Katumba Mnyaki linalomilikiwa na
halamshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi halina choo tangu kuanzishwa
kwake miaka 40 iliyopita hali inayosababisha baadhi ya wafanyabishara
kujisaidia vichakani ambopo muda wowote huenda mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu
ukatokea.
Hayo yamebainishwa na wakazi wa Kata ya Katumba
wanaotumia soko hilo ambapo wamesema wanaishi kwa taharuki ya kukumbwa na kipindupindu kutokana na kukithiri kwa uchafu na ukosefu wa
choo katika soko hilo.
Kwa upande
wao mwenyekiti wa soko hilo Bw.Leonard Kigwasu na Afisa Mtendaji wa vijiji vya
Mnyaki A na B Bw.Kombo Masatu wamekiri kuwepo kwa uchafu sokoni hapo huku
wakisema choo kinatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi miwili ijayo.
Baadhi ya
wamiliki wa maduka ya kibiashara wamesema wanatozwa kuanzia shilingi elfu sita
na mia tano huku wafanyabishara wanaouzia bidhaa chini wakilipa ushuru kila
wanapouza.
Kwa mjibu
wa takwimu iliyotolewa hivi karibuni na Diwani wa Kata ya Katumba Senetor
Braka,jumla ya vijiji 16 vya kata hiyo vyenye jumla ya wakazi zaidi ya elfu
hamsini wanapata huduma ya soko hilo.
Awali soko
hilo lilikuwa likiendeshwa na wakuu wa Ofisi za makazi za Shirika la wakimbizi
Duniani ambapo miaka ya hivi karibuni wakazi hao walipewa uraia wa Tanzania na
soko hilo kuhamishiwa katika mamlaka ya Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments