WAKAZI KATA YA KATUMBA HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO HAWANA MAJI KWA ZAIDI YA MIEZI 6
Na.Issack
Gerald
WAKAZI wa kata ya Katumba Halamshauri ya Wilaya
ya Nsimbo Mkoani Katavi wameilalamikia serikali kwa kutoshughulikia tatizo la
maji kata ya katumba ambapo kwa sasa hawana maji kwa muda wa miezi 6.
Wakazi hao wametoa malalamiko hayo kwa Nyakati
tofauti wakati wakati wakizungumza kuhusu tatizo la maji linalowasumbua kwa
sasa ambapo wamesema limesababishwa na mashine iliyokuwa ikisukuma maji kuharibika.
Mwenyekiti wa jumuia ya watumia maji Bw.Ngeze Joel amekiri kuwepo kwa tatizo hilo akisema tatizo la maji limetokana na kuharibika kwa mashine huku Afisa Mtendaji wa vijiji vya Mnyaki A na Mnyaki B Kombo Masatu amesema baadhi ya vifaa vimenunuliwa ili kumaliza tatizo.

Mwenyekiti
wa kijiji cha Ndui Stesheni Hussein Nasri mahali Mashine hiyo ilipo kwa upande
wake amesema hakuna mwelekeo wa lini ufumbuzi utapatikana.
Kwa mjibu wa Bw.Hussein Nasri Mashine hiyo yenye thamani ya karibu shilingi milioni 80 inasamabaza maeneo ya huduma za jamii kama soko,shule,kituo vya polisi na sehemu nyingene muhimu.
Kwa mjibu wa Bw.Hussein Nasri Mashine hiyo yenye thamani ya karibu shilingi milioni 80 inasamabaza maeneo ya huduma za jamii kama soko,shule,kituo vya polisi na sehemu nyingene muhimu.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments