TCCIA KATAVI : SERIKALI ITAFUTE MFUMO WA KUDUMU KUSIMAMIA SEKTA YA KILIMO,MENEJA MPANDA KATI NAYE ASEMA UZALISHAJI WA TUMBAKU UMEPUNGUA KUTOKA KILO 3.5 - 1.4 MILIONI
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi
CHAMA cha watu wenye kilimo,viwanda
na Biashara TCCIA Mkoani Katavi,kimeishauri serikali kutafuta mfumo wa kudumu
utakaosimamia sekta ya kilimo ikiwemo kusimamia mfumo wa usambazaji wa pembejeo
za kilimo hapa nchini ili wakulima walime kilimo chenye tija kwao kutokana na
matumizi sahihi ya pembejeo hizo ikiwa zitaletwa kwa wakati.
Ushauri huo umetolewa na Katibu
mtendaji wa chama cha watu wenye viwanda ,kilimo na biashara Mkoani Askofu Raban Ndimubenya katika mahpjiano na
waandishi wa habari Ofisini Kwake kuhusu nafasi ya TCCIA katika kusaidia wakulima kutatua changamoto
za kilimo zinazowakabili ikiwemo matatizo ya pembejeo na masoko ya kuuzia
mazao.
Askofu Ndimubenya pia amesema kuwa
wakulima wa tumbaku hawajaingizwa katika chama cha TCCIA na amesema wakulima wa
zao la tumbaku watakaotaka kujiunga na TCCIA Mkoani Katavi watapatiwa nafasi.
Katika hatua nyingine,ikiwa msimu wa
kilimo cha zao la tumbaku ndiyo umewadia,kwa upande wake Meneja wa Chama cha
Msingi cha Ushirika cha Mpanda Kati Bw Amani Rajabu ametoa wito kwa wakulima wa
zao la tumbaku kulima zao hilo kwa kiwango cha shamba atakaloweza kulitunza na
kupata mapato mengi kuliko kulima shamba kubwa na kushindwa kulitunza na
kuambulia mapato kidogo tena isiyo na ubora.
Aidha Bw.Rajabu amesema,uwezo mdogo
wa makampuni yanayonunua tumbaku mkoani Katavi wakati wakulima wakiwa na uwezo
mkubwa wa kulima tumbaku,kunawaathiri wakulima kiuchumi kwa kuwa wana uwezo wa
kulima zaidi ya kiwango kinachohitajika katika kampuni katika manunuzi.
Wakati huo huo Bw.Rajab amesema
kutokana uwezo mdogo wa kampuni kununua
tumbaku kiwango cha uzalishaji kwa wakulima wa zao hiloika chama cha
Msingi cha Ushirika Mpanda Kati kimeshuka kutoka zaidi ya kilo milioni 3.5 hadi
kufikia kilo milioni 1.4.
Awali kabla ya chama cha msingi cha
ushirika Mpanda Kati kilipokuwa hakijagawanywa mwaka 2014 na kupata usajili
mpya,kilikuwa na vijiji 17 vilivyokuwa wanachama ambapo kwa sasa kuna vijiji 11
ambavyo ni Igagala,Ifukutwa
,Majalila,Mpembe,Igalula,Mchaka,Mpolwe,Katonyaga,Milala Shongo,Ngomalusambo,na
Kabungu.
Hata hivyo bado wakulima Mkoani
Katavi wanalalamika kucheleweshwa kwa pembejeo za kilimo wakati wa msimu wa
kilimo na malipo ya fedha za wakulima baada ya mauzo.
Habarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments