SERIKALI YAOMBWA KUWAANGALIA UPYA WATU WENYE ULEMAVU ZANZIBAR
Mkurugenzi Umoja
wa watu wenye ulemavu Zanzibar Asia Abuu Salami ameiomba
serikali na Taasisi mbalimbali za maendeleo nchini,kuwapa kipaumbele
zaidi watu wenye ulemavu na wasiojiweza pindi zinapotokea fursa za
kimaendeleo kwa wananchi.
Amesema
ni vyema Watu wenye ulemavu kupewa haki sawa za kimaendeleo na watu
wengine wasokuwa na ulemavu ili kila mmoja wao ajihisi huru kama wengine kwani
nao wakiwezeshwa wanaweza.
Aidha
Mkurugenzi Asia amebainisha kuwa bado watu wenye
ulemavu wanakabiliwa na changamoto nyingi katika jamiii
ikiwemo ukosefu wa vifaa wanavyotumia kwa shughuli zao za kila siku kama vigari
vya kutembelea,Fimbo,Miwani na kadhalika.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe Hassan Hatibu Hassan
amewashauri watu wenye ulemavu Mkoani humo kuanzisha Jumuiya ya
pamoja itakayowawezesha kurahisisha upatikanaji wa mahitaji yao.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments