MAHAKAMA KUU KENYA YABATILISHA UFUNGAJI WA VITUO VYA HABARI
Mahakama Kuu nchini Kenya imeamuru kuwashwa kwa vituo vya habari vitatu binfasi na serikali na kuiagiza serikali kutoingilia utendaji kazi wa vituo hivyo hadi kesi hiyo itakaposikilizwa kikamilifu.
Siku ya Jumanne matangazo ya vituo vya KTN,NTVna Citizen TV
yalizimwa ghafla na serikali baada ya mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya
kuzima mitambo yao kuepusha vituo hivyo kurusha moja kwa moja mkutano wa
kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga kama Rais wa watu wa Kenya.
Sherehe ya kuapishwa kwa Raila ilichukuliwa na wengi kama
mzaha lakini serikali imeshikilia kuwa kitendo hicho kilikuwa kinakiuka sheria
za nchi hiyo na kwamba ni kosa la uhaini hivyo ilijaribu kuhakikisha taarifa
hiyo haitawafikia Wakenya wengi ambao wangelifuatilia tukio hilo kupitia
matangazo ya luninga
Okiya Omtata ambaye ni muwasilishaji mashtaka na
mwanaharakati amesema anataka agizo la serikali litangazwe kuwa kinyume na
katiba na vituo hivyo vifidiwe.
Wakenya wengi wamekosa matangazo ya runinga kwa siku tatu
sasa huku vituo hivyo vilivyoathirika vikidai kupata hasara ya mamilioni ya
dola za kimarekani.
Vituo hivyo vya binafsi vinategemea fedha za matangazo ya
biashara na hawakuweza kupata fedha hizo kwa siku zote walizokuwa wamefungiwa.
Bw Omtata ametaka serikali ilipie hasara za Citizen TV, KTN
na NTV
Kuibuka kwa mitandao ya jamii kumeathiri vyanzo vya mapato
vya vituo vingi vya habari na kulazimika kuwafuta kazi mamia ya wafanyakazi wao
ndani ya mwaka mmoja uliopita.
Serikali ya Kenya ilitaka vituo hivyo vifungwe hadi polisi
wamalize uchunguzi dhidi ya wanasiasa na waandishi walioshiriki katika sherehe
ya kuapishwa kwa Bw.Odinga siku ya Jumanne ambapo hata hivyo bado haijulikani
kama serikali wataifuatilia agizo hilo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA
LIMITED
Comments