RAIS ASEMA ATAJUA ATAKAVYOFANYA WATAKAOBORONGA MAHAKAMANI, AWABADILIKIA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI PIA WAZIRI WA SHERIA
Rais wa Tanzania Dkt.John Magufuli alisema bado kuna tatizo kubwa katika ofisi ya DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka) na AG (Mwanasheria Mkuu),na ndiyo maana muda mwingine inawapelekea kuwapa changamoto kubwa Majaji.
Kwa
upande mwingine,Rais Magufuli amewataka viongozi wengine wanaosimamia vyombo
vya sheria kufuata mfano mzuri aliyouanzisha Profesa Ibrahimu Juma kwa
kutowafumbia macho wahalifu wa aina yeyote ile.
Rais
ambaye alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hizo aliongozana viongozi wengine wa
serikali.
Wakti
huo huo Rais Dkt.Magufuli leo amewabadilikia Waziri wa Katiba na
Sheria,Prof.Palamagamba Kabudi na Mwanasheria Mkuu wa serikali,George Masaju na
kudai kuwa wanakwamisha haki kutendeka kwa watu kutokana na kutofanyia kazi
mambo ya msingi.
Amesema
yeye ameumbwa kusema ukweli hivyo
ataendelea kuusema hata kama kuna watu unawaumiza.
Wakati
huo huo Rais Magufuli kupitia kilele cha maadhimisho ya 22 ya siku ya Sheria amewapa
pole Majaji kwa changamoto wanazokumbana nazo pindi wanaposhughulikia mashitaka
yanayopelekwa na serikali na kuahidi kulifanyia kazi jambo hilo kabla ya mwezi
Februari kuisha huku akidai ameshajifunza vya kutosha.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments