MTANZANIA AHUKUMIWA KUNYONGWA UGANDA
Mahakama
Kuu nchini Uganda imemuhukumu Mtanzania kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana
na hatia ya mauaji.
Mtanzania
huyo aliyetambulika kwa jina la Matule Chresporeto Coleheri mkazi wa Bukoba
anadaiwa kumuua mfanyakazi mwenzake katika shamba moja lililoko eneo la Wakyuto
wilayani Nakaseke.
Akisoma
hukumu hiyo,Jaji Steven Mubiru amesema baada ya kusikiliza ushahidi uliotolewa
na upande wa mashtaka,mahakama imejiridhisha kuwa Matule ndiye alitenda kosa
hilo.
Amesema
mashahidi watatu walioshuhudia tukio hilo wameiridhisha mahakama kuwa Thomas
Kamuhebwa aliuawa na mtuhumiwa huyo.
Mwili
wa Kamuhebwa ulikutwa ukiwa umetupwa katika shimo moja na kufungwa katika begi
hali iliyosababisha mwili kuokotwa karibu na makazi ya mshtakiwa.
Hata
hivyo,mbele ya mahakama hiyo Matule alijitetea kutohusika katika mauaji hayo na
kudai tuhuma hizo zilitengenezwa na watu waliotaka kuiba magogo yake
aliyoyaandaa kwa ajili ya kuzalisha mkaa.
Awali,ilielezwa
mahakamani hao kuwa Matule ni mhamiaji kutoka Tanzania aliyekuwa akifanya kazi
za vibarua na kwamba Februari 6 mwaka,2014 alimuua Kamuhebwa kwa sababu zisizojulikana
na kufukia mwili wake katika shimo.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments