NDUGU 6 MKOANI RUKWA WAHUKUMIWA KUNYONGWA-Septemba 27,2017
Na.Issack Gerald-Sumbawanga Rukwa
NDUGU sita wa familia moja wamehukumiwa kifo
kwa kunyongwa baada ya kuthibitika Kuwa walimuua ndugu yao wakimtuhumu Kuwa ni
mchawi.
Ndugu hao walihukumiwa Jana na mahakama kuu ya
kanda ya Sumbawanga baada yakuridhika na upande wamashtaka Kuwa walitendakosa
hilo.
Jaji Wa Mahakama hiyo, Dk Adam Mambi
alisoma hukumu hiyo ambapo alisema kuwa pasipo kuacha shaka watuhumiwa
walifanya mauaji ya ndugu yao huyo.
Waliokutwa na hatia katika shauri hilo ni
Ferdinand Kamande, Peter Mpandisharo, Edes Kamande, Stephen Sikanda, Henrick
Nguvumali Anatory Kamande huku watuhumiwa Alistid Kamande na Will broad Kamande
wakiachiwa huru kwa kutokutwa na hatia Katika shtaka hilo.
Katika shauri hilo upande wa mashitaka
uliongozwa na mawakili wa serikali ambao ni Scolastica Lugongo na Adolf Lema
huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na wakili Mathias Budodi, ambapo ilidaiwa
kuwa washitakiwa walifanya mauaji hayo Septemba 27, mwaka 2014.
Awali Ilielezwa mahakamani hapo kuwa siku ya
tukio nyakati za usiku washitakiwa wakiwa na silaha za jadi kama ambazo ni
mapanga, nondo, mawe, majembe walivamia nyumba ya Kamande na kuvunja mlango
ambapo Kamande alikimbia kuelekea kusikojulikana.
Ilielezwa kwamba baada ya hapo waliichoma moto
nyumba hiyo na kuteketeza kila kitu kilichokuwemo ndani kisha kuondoka
zao.
Wakati nyumba hiyo ikiteketea kwa moto Kamande
aliyekuwa amekimbia ili kunusuru maisha yake, ndipo walipomtafuta na kufanikiwa
kumpata na kisha kuanza kumpigwa wakimtuhumu kuwa ni mchawi na baada ya kumpiga
waliamua kumchoma moto hadi kufa.
Ilidaiwa kuwa washitakiwa hao walikamatwa na
polisi Oktoba 10, 2014 na baada ya kuhojiwa na polisi walikana shitaka hilo.
Awali kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo,
mawakili wa Serikali waliiomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho
kwani vitendo vya watu kuua wenzao kwamadai Kuwa ni wachawi vimeanza kukithiri
mkoani humo.
Akitoa adhabu hiyo Jaji wa Mahakama hiyo, Dk
Mambi amesema ameridhishwa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa
mashitaka hivyo kwa kutumia Kifungu cha Sheria ya Makosa ya Jinai Namba 196
Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo 2002 anawahukumu watu hao sita kunyongwa
hadi kufa.
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au Ukurasa P5Tanzania Limited
Comments