CCM WILAYANI MPANDA WAPATA VIONGOZI WAKE JUMUIYA YA WAZAZI,UVCCM NA UWT-Septemba 26,2017
Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
JUMUIYA ya wazazi ya chama cha
Mapinduzi CCM Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,imemchagua Bw.Abdalah Mtwenya
Kapongolola kuwa mwenyekiti atakayeiongoza jumuiya hiyo mpaka mwaka 2022.
Msimamizi wa uchaguzi huo ambao
umefanyika leo mjini Mpanda Bw.Reginald Mhango amewataja wengine
waliochaguliwa kuwa ni na Modesta Mpanda Ngazi mjumbe wa mkutano mkuu
taifa,Yasin Kilimanjaro mjumbe Halmashauri kuu,Leticia Chindiko Mkutano mkuu wa
Mkoa,Michael Nestori Mwakilishi UVCCM mkoa na Bi.Richard Mayaya mwakilishi wa
UWT.
Wengine waliochaguliwa uwakilishi
baraza la wazazi Wilaya ni Eriziel Samweli Fyula,Simon Malima na Joseph
Mpangalilo.
Mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo Bw.Abdalah
Mtwenya Kapongolola pamoja na mambo mengine ameomba ushirikiano Kutoka kwa
wanajumuiya hiyo ili kuendeleza chama na kutunza rasilimali za chama kwa ajili
ya kukuza uchumi wa chama.
Naye katibu wa CCM Wilayani Mpanda
Bi.Elizabeth Kasmili Kibiriti amewapongeza wanachama kutumia nafasi zao
kuchagua viongozi wanaowataka kwa manufa aya chama huku mwenyekiti mstaafu wa
jumuiya hiyo Bw.Abel Hamis Kimazi akiwataka wanachama kushirikiana na viongozi wapya
kuendeleza chama.
Jumala ya kata 27 za wilaya ya Mpanda
zilizokuwa na wapiga kura zaidi ya 246 zimeshiriki uchaguzi huo huku mkutano
ukihudhuriwa na wanachama wa jumuiya hiyo karibu 300 wakiwemo madiwani na
mbunge wa jimbo la Nsimbo.
Kata hizo ni Litapunga, Mkanyagio, Magamba,
Kanoge, Sitalike, Shanwe, Kazima, Nsimbo, Kapalala, Uwanja wa ndege, Mwamkulu, Mpanda Hotel, Kashaulili, Ibindi, Kakese,
Ilembo, Kawajense, Uruwila, Machimboni, Nsemulwa,
Itenka, Misunkumilo, Kasokola, Ugalla, Mtapenda, Majengo na Katumba.
Jumuiya nyingine ambazo jana zimefanya
uchaguzi ili kupata viongozi wake wilayani Mpanda ni Umoja wa Vijana wa chama
cha Mapinduzi CCM (UVCCM) na Umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi CCM
(UWT).
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au Ukurasa P5Tanzania Limited
Comments