MBUNGE JIMBO LA NSIMBO ATUHUMIWA KUJIHUSISHA NA RUSHWA KATIKA UCHAGUZI WA UVCCM WILAYANI MPANDA KATAVI -Septemba 27,2017
Mbunge Jimbo la Nsimbo Richard Mbogo |
Malalamiko hayo yametolewa leo na aliyekuwa
Mgombea kwa nafasi ya mwenyekiti wa vijana Bw.Saimoni John Saimoni katika
uchaguzi uliofanyika jana ambapo amekiri kuwepo kwa vitendo vya rushwa miongoni
mwa viongozi na kusema hali hiyo ndiyo iliyomkwamisha kushinda kiti hicho.
Bw.Simon John Simon amemtuhumu mbunge
wa jimbo la Nsimbo Richard Philipo Mbogo kuwa ni miongoni mwa waliokuwa
wakihusika kutoa rushwa kwa wajumbe wa mkutano hadi shilingi elfu ishirini(20,000)
kwa kila mjumbe aliyekuwa na sifa ya kupiga kura.
Hata hivyo mbunge wa jimbo la Nsimbo Richard
Philipo Mbogo amekanusha madai hayo na
kusema kuwa kama kuna mtu au mgombea mwenye ushahidi wa vitendo hivyo vya
Rushwa aende mahakamani ili kutoa ushahidi huo.
Kwa upande wa Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni Diwani Kata
ya Makanyagio Hidary Sumry amesema uchaguzi huo ulikuwa huru na haki na amewataka
wenye malalamiko kuyapeleka katika vyombo husika.
Uchauzi
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au Ukurasa P5Tanzania Limited
Comments