CHADEMA WAENDELEA NA UCHAGUZI WA VIONGOZI NGAZI YA MITAA-Septemba 27,2017
Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
Chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema)
mkoani Katavi kimewataka wanachama wake kuwa watulivu katika kipindi cha
uchaguzi mdogo unaojulikana kama chadema msingi.
Hayo yamesemwa na katibu wa chama
hicho ngazi ya wilaya Bw.Iddi Omary Faraji
baada ya kutolea ufafanuzi wa sintofahamu kuhusu chaguzi mbalimbali ambazo
zimekuwa zikiendelea katika vyama tofauti.
Aidha katibu ameelezea lengo la
uchaguzi huo kuwa ni kutaka kujua wanachama walioingia pamoja na waliotoka
ndani ya chama hicho.
Hata hivyo amewaomba wanachama
kuonyesha ushirikiano ili kukijenga chama hicho.
Kwa mjibu wa kiongozi huyo,chama cha Demokrasia
na Maendeleo Chadema kinatarajia kufanya chaguzi mbalimbali katika ngazi ya
mitaa mpaka watakapofanya uchaguzi wa kupata viongozi wa kitaifa ifikapo mwezi
Oktoba mwaka 2017
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au Ukurasa P5Tanzania Limited
Comments