WANAFUNZI 417 WAKATISHA ELIMU WILAYANI MLELE-Septemba 27,2017
Na.Issack Gerald-Mlele Katavi
ZAIDI
ya wanafunzi 417 wa sekondari katika halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani
Katavi wamekatisha masomo yao kwa kipindi cha kati ya mwaka 2014 na 2016
kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mimba na utoro
Hali
hiyo imebainishwa na Afisa elimu idara ya Sekondari Bw.Sylivanus Raphael
Kunambi ambapo amesema kuwepo changamoto ya wanafunzi kuikatisha masomo kwa
sababu mbalimbali ikiwemo utoro na mimba.
Kunambi
amesema kwa mwaka 2014 wanafunzi 108 sawa na asilimia 17.4 ya wanafunzi wote
waliokuwa wamesajiliwa katika mwaka huo hawakuhitimu huku mwaka 2015 idadi ya
wanafunzi ambao hawakumaliza masomo yao ikiongezeka na kufikia 160 sawa na
asilimia 22.9 wakati huo kwa mwaka 2016
wanafunzi 149 sawa na asilimia 20 ya wanafunzi wote waliokuwa wamesajiliwa
wakishindwa kuhitimu elimu ya sekonadri..
Aidha
ametaja sababu nyingine inayosababisha wanafunzi kutohitimu elimu ya Sekondari
ni pamoja na jamii ya wafugaji wanaohama hama katika wilaya ya Mlele hali
ambayo inaathiri elimu ya mtoto.
Hata
hivyo wazazi,walezi na jamii imeaswa kutambua nafasi na haki ya mtoto kupata
haki yake ya elimu kama inavyostahili kwa kuwa ni haki yake.
Comments