TFS WASISITIZA KUWATIMUA WANANCHI WANAOVAMIA HIFADHI ZA MISITU-Agosti 23.2017

WAKALA wa huduma za misitu nchini TFS  Mkoani Tabora imeendelea kusisitiza azma yake ya kuwaondoa wananchi wote waliovamia kwenye maeneo ya hifadhi kufuatia uharibifu mkubwa unaofanywa na wananchi hao kutokana na kuendesha shughuli mbalimbali za kibinadamu ambazo zimekuwa zikichangia uharibifu.

Akizungumza Katika Kikao Kilichowakutanisha Viongozi Wa Wakala Wa Huduma Za Misitu Tanzania TFS Na Wadau Wa Misitu Kanda Ya Magharibi Mtendaji Mkuu Wa Wakala Wa Misitu Nchini Profesa Dos Santos Silayo Amebainisha Kuwa Shughuli Za Kibinadamu Ikiwemo Kukata Miti Na Kilimo Cha Kuhama Hama Zinachangia Kuharibu Misitu Ya Hifadhi Ambapo Amesisitiza Kuwa Elimu Ya Umuhimu Wa Kutunza Misitu Ya Hifadhi Itaendelea Kutolewa Kwa Wananchi Ili Kukabiliana Na Tatizo Hilo.
Prof. Dos Santos Pia Amewataka Viongozi Wa  Serikali Za Vijiji Kuacha  Kujichukulia Sheria Ya  Kufyeka Maeneo Ya Hifadhi Na Kuwauzia Wananchi.
Mkuu Wa Mkoa Wa Tabora Bw. Aggrey Mwanry  Amesisitiza Matumizi Ya Nishati Mbadala Majumbani Ikiwemo Gesi Ili Kupunguza Tatizo La Ukataji Mitia Kwa Ajili Ya Kuni Na Mkaa.
Duru Zinaarifu Kuwa Mvua Kunyesha Chini Ya Wastani Ni Matokea Ya Uharibifu Wa Mazingira Ikiwemo Kufyeka Misitu Ya Hifadhi, Kuendesha Kilimo Cha Kuhama Hama Na Kuharibu Vyanzo Vya Maji Hivyo Elimu Ya Kutunza Mazingira Inapaswa Kuendelea Kutolewa Katika Jamii.
Habari zaidi www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA