WAZIRI NCHEMBA ATISHIA KUWAFUTIA URAIA WATANZANIA WABAGUZI-Agosti 23.2017

WAZIRI wa mambo ya ndani Mh.Mwigulu Nchemba ametishia kuwafutia uraia watanzania wapya wa Katumba mkoani Katavi ambao walikuwa wakimbizi kwa muda mrefu kutokana na tabia ya ya baadhi yakubaguana kitaifa na kikanda.
Waziri Mwigulu Nchemba


Waziri Nchemba amesema hayo jana  wakati  alipopita kwenye kambi kuangalia usajili unaendeleaje ambapo amesema  wananchi   hao waliopewa uraia wakitokea burundi wakati wa vita ya kikabila miaka 1972 wamekuwa na tabia ya ubaguzi hata kufikia kushindwa kusaidiana kwenye biashara zao.
Waziri aliwaambia wananchi hao kuwa yeyote atakayeleta mambo ya ubaguzi ikiwa ni pamoja na kubaguana kibiashara  katika jamii hatosita kumfutia uraia alioupata kwani Watanzania hawana mambo ya kibaguzi.
Pamoja na hayo Kiongozi huyo alitumia muda huo kuwataka Watanzania kuwa na utanzania ndani ya mioyo yao na waache tabia ya kutaka kukwamisha kila kitu kinachofanywa na serikali kwa kuweka vikwazo mbele ili vitu visifanikiwe.
Waziri mwigulu aliwasili juzi mkoani Katavi kwa ajili ya kufanya ziara kuhusu mambo mbalimbali yaliyo chini ya wizara yake.
Habari zaidi www.p5tanzania.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA