AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPATA KIPIGO KIKALI-P5 TANZANIA MEDIA INAKUSOGEZEA HIYO
Na.Issack Gerald-Mlele
Mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la Ramadhani Ally (20), mkazi wa Kalovya Inyonga,amefariki
dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya Inyonga kufuatia
kipigo kikali alichokipata toka kwa Ntemwa Kabembenya(26) mkazi wa Ipwaga.
Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri
kidavashari,amesema kuwa tukio hilo limetokea tarehe 23.01.2016.
Kabla ya marehemu kufariki,Marehemu alikuwa
amesimama na dada wa mtuhumiwa aliyejulikana kwa jina la Ngoro Mbogo (12) mkazi
wa Ipwaga ambapo baada ya mtuhumiwa kuwakuta wakiwa wamesimama pamoja huku
wanaongea kitendo kile kilimkasirisha mtuhumiwa ndipo alipoanza kumshambulia
kwa kumpiga kwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake.
Kamanda Kidavashari amesema, marehemu
alifariki dunia baada ya kupelekwa katika
hospitali ya Wilaya Mlele kwa matibabu baada ya kipigo alichokipata tarehe 22.01.2016
Chanzo cha tukio hili ni ugomvi kati ya marehemu na mtuhumiwa ambapo hata hivyo
Jeshi la Polisi linamshikilia mtuhumiwa Ntemwa Kabembenya(26)
na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.
Comments