UJENZI WA BARABARA KIWANGO CHA LAMI KUTOKA MPANDA HADI SUMBAWANGA KUKAMILIKA 2016
Na.
Issack Gerald -Dodoma
SERIKALI
imesema ujenzi wa barabara ya Mpanda hadi Sumbawanga kwa kiwango cha lami
unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2016.
Bungeni Dodoma |
Jengo linalotumika katika vikao vya bunge Mjini Dodoma |
Naibu
waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani amesema hayo leo
bungeni mjini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalum Bi. Anna
Lupembe aliyetaka kujua ujenzi wa barabara hiyo utakamilika lini.
Naibu
waziri Ngonyani amesema ujenzi wa barabara ya Sumbawanga hadi Mpanda
umegawanyika katika sehemu nne, ambazo ni Sumbawanga kanazi kilometa 75,
Kanazi-Kibaoni Kilometa 76. 6, Kibaoni- Stalike kilometa 72 na Stalike-Mpanda
kilometa 36.
Amesema
upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa
sehemu iliyobaki ya Kibaoni hadi Stalike umekamilika na serikali inaendelea
kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi .
Comments