MKUU WA MKOA WA KATAVI ATAKA KILA MKAZI KUWA MLINZI WA MAZINGIRA YANAYOMZUNGUKA
Na.Issack Gerald-Mpanda
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dk.Ibrahim Msengi,amemtaka kila wakazi
wa Mkoa wa Katavi kuwa mlinzi wa mazingira yanayomzunguka.
Wito huo umetolewa jana na Mkuu wa
Mkoa wakati wa uzinduzi siku ya wa upandaji miti kimkoa ambao umefanyika katika
katika Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo, kata ya kanoge kijiji cha Kanoge kitongoji cha barabara ya pili-Kanoge.
Aidha Dk.Msengi amesema kuwa suala la upandaji miti
lisiishie kuonekana katika takwimu za maandishi na badala yake wahakikishe
misitu iliyopandwa inaonekana.
Wakati huo huo amewataka venyeviti wa vijiji na kila
muhusika kuhakikisha hakuna mfugaji anaye hamia bila kufuata utaratibu.
Hata hivyo,Dk Msengi ametaka
uandaliwe utaratibu kukabidhiana na kusimamia
mashamba ya miti na ukaguzi uwe unafanyika kila baada ya miezi mitatu kulingana na ratiba itakavyoelekeza
ili ikitokea miti imekufa ijulikane nani wa kutoa taarifa na sababu ya miti
kufa.
Comments